Arsene Wenger anafikiria kuhusu kustaafu? Huwa inamjia akilini, alafu…

Kocha wa klabu ya Arsenal ya UingerezaArsene Wenger amedumu na klabu yaArsenal kwa zaidi ya miaka 15 toka alipojiunga nayo 1996, Wenger anakuwa kocha wa pili katika historia ya Ligi Kuu Uingereza kudumu na timu kwa muda mrefu baada ya kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Fergusonambaye amestaafu mwaka 2013.

Wenger kushoto akiwa na Ferguson

Kufuatia kustaafu kwa Sir Alex Fergusonmwaka 2013 kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na Wenger lini atastaafu, wengi wanaamini Wengeralikuwa na uwezo wa kuifundishaArsenal kutokana na rekodi alioweka ndani ya miaka tisa ya mwanzo klabuni hapo, Wenger alishinda mataji 7 lakini miaka kumi baadae Wenger ameishia kutwaa mataji mawili pekee rekodi inayotia mashaka kuhusu uwezo wake kwa sasa.

Wengi walitazamia kuwa kuna uwezekekano wa Wenger kustaafu kwa miaka ya hivi karibuni lakini alichojibu kuhusu suala la yeye kustaafu bado linawaacha watu njia panda ya lini atastaafu.

“Kustaafu? ndio wakati mwingine huwa inanijia akilini lakini sio zaidi ya sekunde 5 kwa sababu huwa nahofia…Nataka nifanye vizuri na klabu ili siku nitakapoondoka niiache klabu katika nafasi nzuri ili iweze kuendelea poa”>>>Wenger


Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji
 
Support : hassani bakari haji | Benjamin Template | hancy classic Template
Copyright © 2016. kidudumtu - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by +255755537543
Proudly powered by Benjamin