Klabu ya Arsenal ya Uingereza miaka kadhaa nyuma ilikuwa ni nadra sana kukuta inasajili mchezaji kwa gharama za juu ila kufuatia falsafa za kochaArsene Wenger ambae anaaminika kuwa hakutaka kukubali kuwa soka limebadilika na wachezaji wananunuliwa kwa gharama za juu, yeye alikuwa akiendelea kuwatumia wachezaji makinda na kununua wachezaji kwa gharama nafuu.
Wenger alionekana kuanza kukubali kwamba soka limebadilika baada ya kuwasajili Mesut Ozil kutokea Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 42 mwaka 2013 na kumsajiliAlexis Sanchez kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 35 akitokea FC Barcelona.
Kufuatia mpango wa kuboresha kikosi hicho cha Emirates mkurugenzi waArsenal Lord Harris amethibitisha kuwaArsene Wenger ana uwezo wa kumsajili mchezaji yoyote duniani kwa sasa.
Licha ya Wenger kukubali kuwa Arsenalkwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikishindwa kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza ila Lord Harris amethibitishaArsenal kuwa imetenga bajeti ya pound milioni 200 kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao.
“Arsene Wenger anaweza kumnunua mchezaji yoyote duniani, suala la fedha lilikuwa gumu kwetu wakati tunahamia Emirates lakini sasa tuko huru… katika account ya benki tuna pound milioni 200. Hakuna mpango wa kumsajili mchezaji yoyote isipokuwa kama atapata mchezaji nyota kama Ozil au Sanchez, lakini anaangalia mmoja kati ya wachezaji ambao hawapatikani”>>> Lord Harris