Picha za utotoni za Mario Balotelli, Messi, Kaka na story zao za utotoni.

1. Lionel Messi

Lionel Messi

Alizaliwa Juni 24 1987 Rosario Argentinababa yake Jorge Horacio Messi alikuwa mfanyakazi katika kiwanda cha chumaArgentina na mama yake Celia María Cuccittini alikuwa msafishaji.

Akiwa na umri wa miaka mitano Messialianza kucheza soka katika klabu ya Grandoli ya mtaani kwao ambapo kocha wa timu hiyo alikuwa baba yake.

Lionel Messi

Mwaka 1995 Messi alijiunga katika timu ya vijana ya Newell’s Old Boys ambayo ndani ya miaka minne ilipoteza mechi moja pekee, akiwa na umri wa miaka 11Messi alipata matatizo ya ukuaji, ugonjwa ambao ulikuwa unagharimu matibabu dola 900 kwa mwezi ambayo ni zaidi ya Tsh 1900,000/= kiasi ambacho klabu na familia yake hawakuwa na uwezo wa kugharamia.

Lionel Messi wakati alipokuwa mdogo

Mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona wakati huo Carles Rexachakakubali kukiokoa kipaji cha Messi na kumchukua Messi pamoja na baba yake ili akamuangalie Messi wakati anapatiwa matibabu Barcelona alijiunga La Masiakituo cha kukuzia vipaji vya soka kinachomilikiwa FC Barcelona.

Lionel Messi wakati alipokuwa mdogo

2. Ricardo Kaka

Ricardo Kaka

Ricardo Kaka hakuwa tofauti sana na vijana au watoto wengi wa Afrika ambao huwa na tabia ya kujifunza vitu tofauti tofauti wakati wakiwa wadogo, licha ya kuwa hakutokea katika familia yenye maisha magumu, kipindi ana umri wa miaka 8 aliwahi kucheza tennis kabla ya kuamua kujikita katika soka.

Ricardo Kaka katika muonekano wake akiwa mdogo

Kaka baba yake alikuwa engeneer na mama yake alikuwa mwalimu kwa hiyo suala la fedha kwao haikuwa tatizo kitu kilichomfanya aweze kumudu kupata elimu na kucheza soka… Uwezo wake wa soka ulianza kuonekana akiwa na miaka 15 wakati ambao alikuwa akiichezea timu ya  shule ya Alphaville ndipo klabu ya Sao Paulo ilipomuona na kumpa nafasi ya kujiunga katika Academy yaSao Paulo.

Ricardo Kaka katika muonekano wake akiwa mdogo

Alipokuwa na umri wa miaka 18 Kakaalipata mkasa ambao huenda ungeweza msababishia kuachana na soka baada ya kupata ajali wakati akiwa anaogelea katika swimming pool na kusababisha tatizo katika uti wa mgongo kitu ambacho kingeweza kupelekea apate ugonjwa wa kupooza.

Ricardo Kaka

3. Mario Balotelli

Mario Balotelli

Jina lake kamili ni Mario Barwuah raia waItalia, wazazi wake ni wahamiaji kutokeaGhana, wakati ana umri wa miaka mitatu wazazi wake walishindwa kumtunza na kumtoa katika familia ya kizungu yaFrancesco Balotelli na mkewe Silviawamlee hapo ndipo alipolipata jina lake la Balotelli.

Mario Balotelli wakati alipokuwa mdogo

Balotelli aliwahi kuwalaumu wazazi wake wa kumzaa kuwa walimtelekeza licha ya kuambiwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kumtunza, kazaliwa na kukulia Italia ila kutokana na asili ya wazazi wakeBalotelli alikuwa na uwezo wa kuichezea timu ya taifa ya Ghana kabla ya mwaka 2008 kupewa uraia wa Italia na kutangaza kuwa yeye ni muitaliano.

Mario Balotelli wakati alipokuwa mdogo na ndugu zake

“Mimi ni muitalia, naipenda Italia na siku zote nitacheza timu ya taifa ya Italia”>>>Mario Balotelli

Mario Balotelli

Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji
 
Support : hassani bakari haji | Benjamin Template | hancy classic Template
Copyright © 2016. kidudumtu - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by +255755537543
Proudly powered by Benjamin