Daimond Platnumz na Rais Kikwete wameshinda hizi tuzo Afrika Kusini. (African Achievers awards)

Ni siku saba tu zimepita toka mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz ashinde tuzo ya BEST LIVE ACT kwenye tuzo zilizotolewa na MTV BASE AFRICADurban Afrika Kusini.

Usiku wa July 25 2015 Diamond ameshinda tuzo nyingine kwenye tuzo zaAFRICAN ACHIEVERS AWARDS 2015zilizotolewa Afrika Kusini ambako pia Diamond alihudhuria.

Location kulikotolewa tuzo zenyewe Johannesburg South Africa.

Meneja wake aitwae Salam ndio alikua wa kwanza kuwafahamisha Watanzania kupitia page yake ya twitter ambapo Mtanzania mwingine aliyeshinda tuzo kwenye usiku huu ni Rais Jakaya Kikwete aliyeshinda tuzo ya Uongozi bora na ikapokelewa na Dr. Asharose Migiro huku Diamond akichukua ya Artist of the Year kwa mujibu wa Salam.

Tuzo hizi zimekua zikitolewa kwenye mataifa mbalimbali, mwaka huu 2015 zimetolewa Johannesburg South Africa huku za mwaka 2013 zikitolewa Nairobi Kenya, za mwaka 2014 zilitolewa Accra Ghana.

Ni tuzo ambazo zimekua zikitambua michango mbalimbali ya watu mbalimbali waliofanya bidii au kuleta mabadiliko kwenye jamii yao na zimekua zikitolewa kwenye vipengele mbalimbali kama kwa kampuni za simu,Mwanamichezo wa mwakaMwandishi wa habari wa mwakaKiongozi bora wa mwaka na nyingine.

VIDEO FUPI YA DIAMOND AKIONGEA BAADA YA KUPOKEA TUZO

Ni tuzo ambazo zimetolewa kwa kufata pia mfumo wa kupiga kura ambapo kwenye website yao walitoa nafasi ya mtu kujaza fomu kuhusu na kumpigia kura anaemkubali kwenye vipengele hivi hapa chini.

Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji
 
Support : hassani bakari haji | Benjamin Template | hancy classic Template
Copyright © 2016. kidudumtu - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by +255755537543
Proudly powered by Benjamin