Nimeona nikusogezee moja kati ya rekodi ambazo klabu ya Arsenal iliwahi kuziweka mwaka 2004 chini ya kochaArsene Wenger ambaye yupo hadi sasa akiifundisha klabu hiyohiyo… Wengerbado ana heshima ya kipekee Emirateslicha ya kuwa kwa miaka ya hivi karibuni hajaleta mafanikio makubwa kwenye Klabu hiyo.
May 2004 waratibu wa Ligi Kuu Uingereza walilazimika kutengeneza Kombe maalum la Ligi Kuu kwa ajili ya Klabu ya Arsenal, hiyo ilifanyika baada yaArsenal kuandika rekodi ya kumaliza msimu bila kufungwa hata mechi moja msimu wa 2003-04.
Upekee wa Kombe walilopewa Arsenalmsimu huo ilitokana na Bodi ya Ligi Kuu kuandaa Kombe lenye material ya dhahabu, hii ilikuwa tofauti kabisa na haikuwahi kufanyika kitu cha aina hiyo siku za nyuma na halikuwahi kutolewa Kombe la aina hiyo tena mpaka sasahivi.
Hata hivyo huo ulikuwa ni wakati ambao kikosi cha Arsenal kilikuwa kikibebwa na mastaa kama Thierry Henry, Patrick Vieira, Dennis Bergkamp, Nwankwo Kanu, Robert Pires, Ryan Smith, Sol Campbell na Reyes na wengine wengi huku makocha wakiwa Arsene Wengerna msaidizi wake Boro Primorac.