Kwa sare ya Azam FC vs JKT Ruvu, Yanga sasa inahitaji point tatu kuwa Bingwa

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo May 4 2016 kwa klabu ya Azam FCkucheza mchezo wake wa 27 wa Ligi Kuu dhidi ya klabu ya JKT Ruvu na kubakisha michezo mitatu ya Ligi ili kuweza kumaliza msimu wa 2015/2016.

Azam FC wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex Mbande Chamazi, wamelazimishwa sare ya goli 2-2 na JKT Ruvu ambayo kabla ya mchezo huo ilikuwa nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu, yaani ipo katika nafasi ya timu tatu za Ligi zinazoweza kushuka daraja mwisho wa msimu.

Mchezo ulikuwa mwepesi kwa Azam FCambao awali walianza kufunga magoli mawili dakika ya 31 kupitia kwa  Michael Balou baadae dakika ya 37 Kipre Tchetche akafanikiwa kufunga goli la pili kwa Azam FC, wakati JKT Ruvu walianza kusawazisha magoli yote mawili kuanzia dakika ya 56 kupitia kwa Saady Kipangana dakika ya 72 kupitia kwa Mussa Juma.

Kwa matokeo hayo Azam FC sasa inakuwa kama imejiondoa katika mbio za kuipiku Yanga katika nafasi ya kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu bara msimu wa 2015/2016, kwa sasa Azam FC na Yangawatakuwa wamepishana point 8, lakini kila mmoja ana mechi tatu, Yangawakishinda mechi yao inayofuata rasmi watakuwa Mabingwa wa Ligi.

Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji
 
Support : hassani bakari haji | Benjamin Template | hancy classic Template
Copyright © 2016. kidudumtu - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by +255755537543
Proudly powered by Benjamin