Hii kauli nimeinasa kwenye siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo Waziri wa habari, sanaa utamaduni na michezo Nape Nnauye alialikwa na kusimama mbele ya Wadau na Wanahabari na kuyaeleza yafuatayo.
‘Ni ngumu kusimama hapa nisizungumze habari ya bunge live, sio sahihi kusema uamuzi wa kubadilisha namna shughuli za bunge zinavyotangazwa kwamba ni uamuzi wa serikali, huu ni uamuzi wa bunge kama muhimili mmojawapo wa dola uliohuru… nimelisema sana bahati mbaya halijachukuliwa kama tulivyolieleza’ – Nape
‘Uamuzi huu wa kuanzisha studio ya bunge na utengaji wa pesa za kuanzisha studio ya bunge ni uamuzi uliopitishwa na bunge lililopita wakati serikali ya awamu ya tano Nape hakuwemo, inawezekana wakati wa kuupitisha watu hawakuwaza kwa undani kuhusu matokeo ya kupitisha uamuzi huu yatakuaje, sasa matokeo yametokea kila mmoja ameanza kupiga kelele’
‘Sisi kama serikali tunapata tabu kutousimamia ule uamuzi, tunachoweza kufanya tuko tayari kama serikali kukaa katikati ya wadau na bunge tukaweka hoja mezani kupitia mapungufu yaliyopo kwenye mfumo huu na kutafuta namna ya kuyarekebisha badala ya kufunga milango kabisa, undeni timu mje Dodoma tuone tunaweza kufanya nini‘ – Nape Nnauye
‘Wadau undeni timu nzuri ije Dodoma ipitie studio ya bunge na kuona namna inavyofanya kazi ikutane na Wabunge na Wanahabari Dodoma alafu tuorodheshe mapungufu, sisi serikali na bunge na nyie tukae pamoja tuyapitia mapungufu tuone namna ya kushughulika nayo‘