BAADA YA KUTEMANA NA MCHUMBA WAKE, SASA WOLPER AINGIA KATIKA UGOMVI WA KUGOMBEA PEDESHEE WA KIKONGO.


KUCHAMBANA, kutoleana lugha chafu ndiyo ishu iliyopo kwa sasa kati ya nyota wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011 iliyomtoa mlimbwende Salha Israel, Husna Maulid kufuatia madai kwamba, wanamgombea mwanamume Mkongo aliyejulikana kwa jina moja la Mwami.
Nyota wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper katika pozi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Husna ndiye aliyeanza kuwa na uhusiano na Mkongo huyo mwaka jana na kila anapofika nchini hutanua naye kwenye ‘viwanja’ mbalimbali.
“Husna ndiye mwenye mwanaume, akija Bongo wako wote, lakini hivi karibuni ghafla tu, jamaa kaja na kuwa na Wolper, Husna kapigwa chini, sijui Wolper alimpatia wapi?” kilisema chanzo hicho.
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilimtafuta Husna na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alifunguka kwa kusema:
“Ni kweli kabisa, Wolper amenichukulia mwanaume wangu. Mi nimemshangaa sana. Halafu eti ananitumia meseji za ajabu ajabu mimi, eti anasema hajanichukulia bali ni bwana ‘ake siku nyingi (huku akionesha meseji hizo).

 
Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011, 'mlimbwende' Husna Maulid.
Baadhi ya meseji hizo zinaonesha Husna akijibu mapigo upande wa pili huku akishambulia kwa maneno makali kufuatia madai kwamba anatembea na Mkongo wake.
“Jana (Ijumaa) alikwenda naye hoteli…(anaitaja jina) iliyopo Masaki (Dar), wakala chakula kisha wakaenda kulala hoteli… (pia anaitaja jina). Mimi najua kila kitu,” alisema Husna akionesha hasira.
Kwa mujibu wa Husna, awali siku hiyo alitaka kwenda kumfumania Wolper na Mkongo huyo kwenye hoteli waliyokuwa wakila chakula lakini machale kama yalimcheza wakaondoka.

Baada ya kuzungumza ana kwa ana na Husna, Uwazi lilimsaka Wolper kwa njia ya simu ili kumuuliza lakini hakupokea. Wakati mwingine simu yake ilipopigwa ilionekana kuwa bize.
Hata hivyo, ili kumpa nafasi zaidi ya kujieleza, Wolper alitumiwa meseji saa 5:05 asubuhi ikiwa na mashitaka yote ambapo ‘ilideliva’ kwenye simu yake, lakini pia hakuijibu mpaka saa 10:13 jioni wakati gazeti hili linakwenda mitamboni.
Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji
 
Support : hassani bakari haji | Benjamin Template | hancy classic Template
Copyright © 2016. kidudumtu - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by +255755537543
Proudly powered by Benjamin