Shirika la ndege nchini[ATC]limeanza safari za anga kutoka Dar es Salaam na Mbeya Machi 17 mwaka huu.
Safari
ya kwanza ya ndege hiyo imezinduliwa rasmi na Mkurugenzi Msaidizi wa
Biashara Juma Boma ambaye amesema kwa kuanzia shirika lake litafanya
safari nne kwa juma kwa gharama ya shilingi laki moja na elfu hamsini tu
kwa safari moja ya kwenda.
wanazo
ndege bora ambazo wasafiri watafurahia huduma zake wawapo safarini,
Boma amesema shirika lake limejipanga vema kukabiliana na ushindani
uliopo .
Pia
amesema kuwa shirika lake limezingatia matakwa ya wateja hivyo ndege
zake zitaanza safari Dar es Salaam saa sita mchana na kufika Mbeya saa
saba mchana ili kuwawezesha abiria wanaotoka nchi jirani kusini mwa
Afrika kuwahi safari ili kutumia ndege za ATC.
Aidha
Patrick Itula ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa Ufundi wa shirika hilo
amesema hivi sasa Mkoa wa Mbeya unazo fursa za kukuza biashara kupitia
shirika lake kutokana kuwa na mpango wa kuunganisha safari zake kutoka
Mbeya na kwenda mikoa ya kaskazini na kanada ya ziwa.
Itula
amesema kuwa pia wana mpango wa kuanzisha safari za kwenda Congo na
Zambia kupitia Mbeya ili kuimarisha zaidi biashara ya utalii kwani Mkoa
wa Mbeya una vivutio vingi hivyo Mkoa utatumia fursa kujitangaza.
Kwa
upande wake Rubani wa ndege hiyo Richard Shaidi ameipongeza serikali
kwa kukamilisha uwanja huo kwani ni mzuri na umekuwa miongoni mwa
viwanja bora nchini na unaweza kutua wakati wowote kutokana na kufungwa
vifaa vya kisasa.
Na Mbeya yetu
|