Usiku wa Mei 2 2016 ndio ulikuwa usiku wa kihistoria kwa klabu ya Leicester Citytoka ianzishwe miaka 132 iliyopita, huenda unafahamu kamaLeicester wametwaa Ubingwa lakini hujui kama Ubingwa huo ndio Ubingwa wao wa kwanza katika historia ya klabu hiyo. Mtu wangu wa nguvu naomba nikuletee mambo 10.
1- Kabla ya kutwaa Ubingwa msimu Leicester City ilikuwa haijawahi kutwaa Ubingwa wa Uingereza.
2- Mafanikio yake makubwa EPL ni kushika nafasi ya pili mara moja msimu wa 1928/1929
3- Leicester imekuwa ikipanda na kushuka Ligi Kuu Uingereza katika vipindi 13.
4- Msimu wa 2012/2013 Leicester City walitinga nusu fainali ya Ligi daraja la kwanza na walicheza na Watford.
5- Msimu wa 2013/2014 walifanikiwa kupanda daraja na kushiriki EPL msimu wa 2014/2015.
6- Baada ya kupanda EPL na kushiriki msimu wa 2014/2015 walimaliza wakiwa nafasi ya 14 kabla ya hapo robo ya msimu walikuwa nafasi ya mwisho katika hatari ya kushuka daraja.
7- Msimu wa 2014/2015 Leicester walikaa nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi kwa siku 140 na kuweka rekodi ya katika historia ya EPL.
8- Kocha wao Claudio Ranieri amewahi kufundisha vilabu 14 vikiwemo vilabu vya Chelsea, Atletico Madrid na Inter Milan hakuwahi kushinda taji la Ligi Kuu.
9- Claudio Ranieri wakati anaingia kuifundisha Leicester City hakuwahi kupewa imani na wachambuzi wa soka Uingereza kutokana na CV yake ya vilabu alivyofundisha.
10- Kauli ya kwanza ya Claudio Ranieri baada ya kupewa kibarua hicho “Nilisema ni ngumu sana kupata mafanikio Ligi Kuu ndani ya msimu wa pili Ligi Kuu, malengo yangu ni kuhakikisha namaliza msimu nikiwa na point 40 tu”
CHANZO: AZAM TV